Our Services

USAFI WA MAJUMBANI

Kikundi kinajihusisha na usafi wa ndani na nje ya nyumba. Usafi huu ni pamoja na ufagiaji, ufutaji, utunzaji wa bustani n.k. Kikundi kinatoa huduma hii ya kuweka mazingira ya nyumba salama na safi kwa kiwango cha juu.

USAFI WA MITAANI

Kikundi kinajihusisha na usafi wa ndani na nje ya nyumba. Usafi huu ni pamoja na ufagiaji, ufutaji, utunzaji wa bustani n.k. Kikundi kinatoa huduma hii ya kuweka mazingira ya nyumba salama na safi kwa kiwango cha juu.

USAFI WA MAOFISINI

Kikundi kinajihusisha na usafi wa maofisini. Kikundi kinafanya kazi ya kusafisha ofisi za umma na binafsi. Usafi unaofanywa na kikundi ni pamoja na ufagiaji, ufutaji, utunzaji wa bustani n.k.

About Us

HISTORIA YA KIKUNDI

Wazo la uanzishwaji wa kikundi liliibuka kama moja ya stori zilizopigwa msibani baina ya watu wawili waliokutana kuomboleza msiba wa mzee mmoja aliyefariki mwezi Novemba, 2019, Mwenge, Dar es Salaam.

Katika stori hizo; umoja uligunduliwa kuwa nyenzo muhimu ya jamii ya vijana waliokuwa Mwenge ili kunufaika fursa zitakazotengenezwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa stendi ya mabasi na uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa katika eneo lao. Hivyo kupelekea uanzishwaji wa kikundi cha Juhudi Mwenge Group tarehe 20 Novemba,2022.

Why Choose Us

SHUGHULI ZETU

Juhudi Mwenge Group ni kikundi cha vijana cha kijamii kilichopo Mwenge Kijijini, Kata ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam kilichosajiliwa na Manispaa ya Kinondoni tarehe 7 Disemba 2022 kwa namba KMC/YGR/3274 ili kutoa huduma zifuatazo:-
• Ulinzi wa Mali binafsi za watu mbalimbali, • Usafi wa Mazingira na • Ukusanyaji Ushuru sehemu za Biashara, bada, Burudani na Makazi.

DIRA, DHAMIRA NA MALENGO

a) Dira ya Kikundi
Kikundi kinatazamia kukuza uchumi wa vijana waliopo Jijini Dar es Salaam.
b) Dhamira ya Kikundi
Kikundi kinalenga kuwezesha mazingira mazuri ya Biashara, Ibada, Burudani na Makazi; kwa kutoa huduma thabiti za Ulinzi wa mali, Usafi wa Mazingira na Ukusanyaji Ushuru.
c) Malengo ya Kikundi
Malengo ya kikundi ni kutoa huduma za Ulinzi wa Mali binafsi za watu mbalimbali, Usafi wa Mazingira na Ukusanyaji Ushuru sehemu za Biashara, Ibada, Burudani na Makazi.

Misingi Mikuu

Katika uendeshaji wa shughuli zake Juhudi Mwenge Group inazingatia mambo makuu sita (6) ambayo ni:-
Ubunifu:-Mawazo mapya na maboresho ya shughuli zetu ni msingi wa utendaji wetu.
Uaminifu:-Tunasimama katika kweli kwa shughuli na mienendo yote.
Uwajibikaji:-Tunawajibika kwa wadau wetu wote kutokana na matendo yetu.
Umoja:-Sisi ni wamoja na kazi zetu tunafanya pamoja.
Ufanisi:-Tunatumia rasilimali stahiki kwa kila lengo tulilopanga.
Uwazi:–Shughuli na taarifa zetu zipo wazi kwa kila muhusika.

Uongozi

Uongozi wa kikundi upo chini ya Kamati Kuu inayoongozwa na Mwenyekiti na Kamati Tendaji inayoongozwa na Katibu. Mwenyekiti ni msimamizi wa kikundi kwa niaba ya wanakikundi. Katibu ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli zote za kikundi.

Our Team

Twaha S.Twaha

KATIBU

Gasper M.Daru

MJUMBE

Yahaya A. Mgalike

DRIVER

Ramson E.Fongo

DESIGNER

What says our Customers

Info

umoja uligunduliwa kuwa nyenzo muhimu ya jamii ya vijana waliokuwa Mwenge ili kunufaika fursa

Subscribe